Madrasatul-khaleej ilianzishwa mnamo mwaka 1995 ilala nyumba no 38. Mpaka sasa madrasa imefikisha miaka 29.

Madrasatul-khaleej makao yake makuu ni Dar es salaam Ilala Tanzania. lakini ina matawi yake sehemu mbali mbali ndani ya mkoa wa Dar es salaam kama vile:

Ilala – Tanga & Kigoma No 41 (Wasichana )

Ilala – Morogoro & Kilwa No 47 (Wavulana )

Kariakoo – Mkunguni & Nyasa No 8.

Temeke – Boko No 66.

Kigamboni – Mwera magengeni No 05

Ukonga madafu – Sababa No 24 .

Kazi za madrasatul khaleej:

Madrasatul khaleej imejikita katika kufundisha elimu ya dini ya kiislamu katika aina zifuatazo (Taalim na Tahfeedh):-

a) Taalim (watoto kuanzia umri wa miaka 3 )

  • Raudhwa (shule ya awali )(miaka 3-6)
  • Ibtidai (primary school )(miaka 7-13)
  • Mutawasitwa ( midole school )(14-17)
  • Thanawi (High school )(18-21)

NB:Utaratibu huu unawahusu watoto walioanzia kusoma madrasatul khaleej,ama watoto wanao hamia kutoka madrasa zingine watapangiwa madarasa kwa kuzingatia matokeo yao ya intervew na si umri wao.

b) Tahfeedh.

kwa watoto kuanzia umri wa miaka 7-10 wanahifadhi kwa muda wa miaka miwili mpaka mitatu.

Na kwa watoto wenye umri wa miaka 11-15 wanahifadhi kwa muda wa mwaka mmoja na nusu mpaka miwili.

Pia kuna kitengo maalumu cha madrasa ya kina mama na mabinti walio maliza darasa la saba,kitado cha nne,kidato cha sita na chuo kikuu.

wanafunzi wa kitengo hiki wanasoma kwa njia mbili sifuatazo;

  • Njia ya kuhudhuria darasani
  • Njia ya online

Pia kuna kuna shule ya awali (Al khaleej DayCare Center) kwa watoto kuanzia umri wa 2-5 iliyopo mtaa wa mwanza na nzasa nyumba no 17.